Kitaifa

MKEMI: Simba tushangilieni kesho ila Jumapili moto ule ule

on

MJUMBE wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi amesema hata mashabiki wa Simba wajae vipi uwanjani kesho kuishangilia Yanga wasitarajie Wanajangwani hao watalipa fadhila kwa kufanya hivyo katika mchezo wao wa kombe la Shirikisho dhidi ya Gendarmerie Nationale FC ya Djibout Jumapili hii.

Kauli hiyo ya Mkemi imekuja siku moja baada ya msemaji wa Simba Haji Manara kuwasihi mashabiki wa timu hiyo kutoizomea Yanga itakayopambana na St. Louis ya Shelisheli katika mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika hapo kesho, badala yake waiunge mkono kwavile hii ni michuano ya kimataifa na timu hiyo inaliwakilisha taifa la Tanzania.

Akizungungumza na wanahabari leo kuhusiana na maandalizi ya mchezo wao wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya St. Louis ya Shelisheli, Mkemi alisema hawatoishangilia Simba kwavile hakuna faida ya kufanya hivyo kwani waliwahi kujaribu lakini Wekundu hao waliishia kuwaaibisha kwa kukubali kichapo toka kwa wageni.

“Sisi ndio tulianza utamaduni huo lakini tumeona haina maana kwasababu watu wenyewe tukienda kuwashangilia wanafungwa, 1992 tulienda kuwashangilia lakini wakatuaibisha sasa tunawapa sapoti ya nini watu kama hao?. Nasema haitawezekana kuishangilia Simba.” alisema Mkemi.

Katika hatua nyingine, Mkemi amesema uongozi wa Yanga umesikitishwa sana na kitendo cha wasimamizi wa Uwanja wa Taifa kuwazuia kufanya mazoezi uwanjani hapo jana kwa kile kilichoelezwa kuwa uwanja huo si wa mazoezi bali ni kwa ajili ya mechi tu.

Mkemi alisema Yanga imekuwa haitendewi haki katika matumizi ya uwanja huo kwani tangu ufunguliwe baada ya kufanyiwa matengenezo, wao wamepata nafasi ya kucheza mechi moja tu tena wakiwa wageni lakini simba wamepata nafasi ya kucheza mechi nne.

“Sisi tumeomba kufanya mazoezi tumekataliwa wakati sisi tunaiwakilisha nchi tena klabu bingwa, tangu ufunguliwe tumepata nafasi ya kucheza mechi moja pekee lakini wenzetu wanaoshiriki kombe la shirikisho tu wanapewa uwanja kila mara, kwenye mechi zao za ligi mzunguko wa pili karibu zote wamechezea uwanja wa Taifa hilo limetusikitisha sana.” alisema Mkemi.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Akram Msangi

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *