Burudani

Mtoto wa Ray aonekana kwa mara ya kwanza

on

MSANII wa filamu wa siku nyingi Vicent Kigosi ‘Ray’, kwa mara ya kwanza leo ameonyesha picha ya mtoto wake baada ya mwaka mzima kupita toka kuzaliwa kwake.

Ray alijaliwa kupata mtoto wake wa kwanza na muigizaji mwenzie Chuchu Hans mwanzoni mwa mwaka jana na kumpa jina la Jaden.

Msanii huyo zao la Kaole Sanaa Group toka ampate Jaden hakuwahi kuonyesha picha yake mahali popote, hivyo kufanya baadhi ya mashabiki wake waanze kuhoji mitandaoni wakionyesha hamu ya kuona sura ya mtoto huyo.

Picha ya mtoto huyo imeibua hisia za watu wengi akiwemo miss Tanzania 2006 na muigizaji maarufu nchini Wema Abraham Sepetu ambaye aliiposti katika ukurasa wake wa Instagram.

Ray ambaye ni staa huyo wa filamu ya Johari ameweka picha ya mtoto wake huyo kwenye ukurasa wake wa Instagram na kupokea maoni tofauti kutoka kwa mashabiki wake.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Zuhura Hassan

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *