Burudani

Muonekano mpya wa Ruby wazua utata mtandaoni

on

MSANII wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini Ruby, amezua gumzo katika akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram leo baada ya kutupia picha zake zikionyesha muonekano mpya kuanzia Januari mwaka huu.
Nyota huyo aliyeibuliwa na kituo cha kukuza vipaji cha (THT), ameweka picha zake zinazomuonyesha akiwa ameongezeka maumbile yake kwa kiasi kikubwa hasa kwenye makalio tofauti na alivyokuwa awali.
Picha hizo ziliwashangaza watu wengi kutokana na muonekano huo mpya anaodai kubadilika baada ya mwaka kuanza.
Muonekano huo umeibua hisia tofauti kwa wapenzi na mashabiki wake ambapo wengi wao hawajaamini na kusema ni picha zilizohaririwa huku wengine wakiishia kupigwa butwaa.
Mkali huyo anayetamba na ngoma yake ya ‘Na Yule’ alituma picha hiyo aliyoandika maneno haya “Mapenzi yanakondesha sana, ila ukimpata mwandani ni furaha”
huku nyingine akiandika “Happy new year na mambo mapya”
 
USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Zuhura Hassan

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *