Habari za kuaminika za michezo na burudani kila wakati.

Mwakyembe amrejesha King Majuto Muhimbili

Kufanyiwa vipimo upya kabla ya kupelekwa India

0 81

WAZIRI mwenye dhamana ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa serikali imeamua kumrudisha nguli wa filamu nchini, Mzee Majuto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ili aweze kufanyiwa vipimo upya kujua kinachomsumbua.

Mzee Majuto alikuwa akipatiwa matibabu katika hopitali ya binafsi ya Tumaini ambapo sasa waziri Mwakyembe amesema wameona ni vema akafanyiwa vipimo tena ili ipatikane ripoti mpya kabla hajasafirishwa kwenda nchini India kwa matibabu.

Related Posts
King Majuto

Wakati akisubiri kusafiri kwenda nje ya nchi (India) kati ya Jumatatu na Jumanne kwa ajili ya matibabu tumeamua tumuhamishie kwanza Muhimbili ili afanyiwe vipimo zaidi, lakini niwaambie mashabiki wake na Watanzania kwa ujumla kuwa Mzee Majuto anaendelea vizuri.

Majuto amekuwa akiugua kwa muda mrefu ambapo sasa serikali imeamua kulivalia njuga suala lake ikiwemo kuhakikisha makampuni yaliyofanya kazi na mkongwe huyo yanatoa msaada ili kuhakikisha afya yake inaimarika.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.

Comments
Loading...