Kitaifa

Mzee Akilimali atajwa kuwa chanzo cha kuvunjika kwa mkutano Yanga

on

BAADA ya jana Jeshi la Polisi kupiga ‘stop’ mkutano wa matawi wa Yanga, imeelezwa chanzo ni Katibu wa Baraza la Wazee wa klabu hiyo Ibrahim Akilimali na jopo lake.

Jana Jeshi la Polisi lilizuia mkutano huo uliotarajiwa kufanyika Makao Makuu ya klabu hiyo Jangwani Jijini Dar es Salaam huku wanachama wakipigwa na butwaaa baada ya kuona Polisi wakifurika klabuni hapo.

Habari za kuaminika kutoka kwa mmoja wa viongozi wa matawi ya klabu hiyo, zinasema kuwa Akilimali na wenzake baada ya kubaini mkutano huo ungewajadili waliamua kutimkia Polisi na kudai kuna viashiria vya uvunjifu wa amani.

Mtoa habari huyo alisema, Akilimali amekuwa akivuruga amani ndani ya klabu hiyo  wakati anatambua wanakabiliwa na tatizo la uchumi linalopelekea hata wachezaji na viongozi kutolipwa mshahara kwa wakati.

“Unajua huyu Akilimali ni mtu mdogo tu ndani ya Yanga kwa nini anatuvuruga?, na ni kweli tulitaka tumjadili halafu tupeleke maoni yetu kwa Kamati ya Utendaji ambayo ingeyawasilisha kwenye Mkutano Mkuu Februari,” alisema.

BOIPLUS iliwatafuta baadhi ya viongozi wa matawi ili kujua ukweli zaidi juu ya tukio hilo. Bakili Makele alikiri habari za Akilimali kwenda Polisi kuzuia mkutano wao baada ya kujua watamjadili kitu ambacho ni kweli kwani alikuwa moja ya ajenda ambazo wamezizungumzia kutokana na tabia yake aifanyayo.

“Wale wazee wana ajenda zao za kuivuruga Yanga na kweli kabisa walienda kutoa ripoti Polisi kuwa mkutano unaweza kuwa na vurugu. Kwa kuwa Polisi ni watu wa kulinda amani wakaja kujiridhisha,”

Mbali na hilo alisema, walitaka kujadili jinsi gani watapata pesa kutokana na ukata walionao, wajadili jinsi ya kuingia katika mfumo mpya wa hisa na mengineyo. Hata hivyo mwandishi wa habari hii alimtafuta Akilimali ili azungumzie tuhuma hizo na akasema kuwa hajafanya kitu kama hicho kwa maelezo kuwa wamejizuia wao wenyewe wasimsingizie.

“Hapana sijafanya jambo hilo, wao wenyewe ndio wamejizuia wasinisingizie mimi bwana,” alisema Akilimali huku akicheka kwa nguvu.

Naye Mwenyekiti wa Tawi la Yanga Uhuru Kais Mwasongwe alisema, wana imani mkutano wao utafanyika kwani tayari Waziri mwenye dhamana ya michezo Harrison Mwakyembe ameishauandikia barua uongozi wao ili wawaruhusu wafanye na Polisi wakalinde amani.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Clezencia Tryphone

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *