Kitaifa

Niyonzima atuma salamu kwa wachezaji wenzake Simba

on

KIUNGO wa Simba Haruna Niyonzima amewataka wachezaji wenzake kupambana ili kutwaa kombe la michuano ya Mapinduzi inayoendelea kutimua vumbi Visiwani Zanzibar.
Michuano ya Mapinduzi ilianza Disemba 29 mwaka jana, huku ikitarajiwa kufikia tamati Januari 13, ambapo inazikutanisha timu mbalimbali za Bara na Visiwani.
Niyonzima ambaye ana maumivu ya enka kwa sasa, aliiambia BOIPLUS leo kuwa anatambua hakuna mashindano mepesi, hivyo ni jukumu la wachezaji wenzake kuhakikisha wanajituma na kupambana ili kurejea na kombe la michuano hiyo.

Niyonzima wa pili kushoto akifanya mazoezi na wenzake (picha ya maktaba)

“Nawaomba wachezaji wenzangu wapambane mimi naumwa, natamani sana ningecheza ila ni majaliwa ya Mungu,katika mpira hakuna mashindano mepesi, kitu kikishaitwa mashindano kinahitajika jitihada kubwa sana,”alisema.
Aidha Niyonzima aliwataka mashabiki wa timu hiyo kumuombea dua ili aweze kurejea mapema dimbani na kuendeleza mapambano kwani anatambua Simba ina majukumu mengine ikiwemo michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Simba inatarajia kushuka dimbani kesho kuwakabili mabingwa watetezi wa kombe hilo Azam FC ambao muda mfupi baadae watashuka Dimbani kuwavaa URA.
Bofya picha hii hapa chini ku’SUBSCRIBE kwenye chaneli yetu ya YouTube.
USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Clezencia Tryphone

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *