Habari za kuaminika za michezo na burudani kila wakati.

NMB yamwaga vifaa timu za majeshi

0 880

BENKI ya NMB imetoa vifaa vyenye thamani ya Tsh. Milioni 10 kwa timu za Majeshi ambazo zinajiandaa na mashindano ya Majeshi yanayotarajia kuanza Mei 8 hadi 20 mwaka huu kwenye viwanja vya Uhuru na Twalipo Jijini Dar es Salaam.

Michezo mbalimbali ikiwemo soka, netiboll,  riadha, ngumi, kulenga shabaha na mpira wa mikono inatarajiwa kuwepo na washindi watazawadiwa zawadi mbalimbali.

Akizungumza kwenye Hafla ya kukabidhi vifaa hivyo Meneja Mwandamizi na Mahusiano kwa Wateja wa NMB, Gibson Mlaseko alisema kuwa sababu ya kutoa msaada huo ni kutokana na mahusiano mazuri waliyokuwa nayo na JWTZ katika mambo ya michezo.

“Nashukuru kwa mahusiano mazuri kati yetu na JWTZ kwani hii ni mara ya tatu tunasaidiana nao katika masuala mbalimbali ya michezo, pia lengo la msaada huu ni kutambua umuhimu wa michezo kuwa ni kuibua vipaji kujenga afya na ajira hivyo tunaamini wenzetu watavitumia vifaa hivi vizuri na kufikia malengo,” alisema Mlaseko.

Kwa upande wake Luteni Kanali David Mziray, aliishukuru NMB kwa msaada huo na kusema watahakikisha wanavitumia vizuri ili kutimiza malengo ambayo wamejiwekea katika mashindano hayo.

“Tunawashukuru NMB kwa msaada huu, vifaa hivi vitaongeza chachu ya mashindano yetu ambayo hufanyika kila mwaka. Tunaomba na makampuni mengine yaige mfano wao ili kuinua michezo nchini,” alisema Mziray.

Vifaa vilivyo tolewa ni pamoja na mipira ya michezo yote, jezi za michezo mingine yote ambayo itashindaniwa katika michuano hiyo ambayo hufanyika kila mwaka.

⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽

Get real time updates directly on you device, subscribe now.

Comments
Loading...