Kitaifa

NUSU FAINALI MAPINDUZI: Makocha ni ‘Full’ kuogopana

on

WAKATI mashabiki wa soka wakisubiri kwa hamu kutazama mitanange ya nusu fainali ya kombe la Mapinduzi leo tena wengi wao wakitambiana, hali ni tofauti kwa makocha wa timu hizo amboa wameonyesha kuhofiana sana.

Yanga kwa upande wao wamekiri mchezo wao dhidi ya URA utakuwa mgumu na wenye ushindani mkubwa hasa baada ya watoza ushuru hao wa Uganda kuzifunga timu kali za Simba na Azam FC.

Yanga inatarajia kushuka dimbani saa 10:30 jioni ya leo kuwakabili URA katika mechi ya nusu fainali ya kwanza huku saa 2:15 usiku bingwa mtetezi Azam ikitarajiwa kupepetana na Singida United iliyoonekana imejipanga kufanya maajabu kwa kutwaa kombe hilo katika ushiriki wao wa mara ya kwanza.

Kocha msaidizi wa Yanga Shadrack Nsajigwa alisema kuwa wanatambua URA ni timu nzuri na imethibitisha ubora wao kwa kuwafunga Simba na Azam ambao ni wazuri pia.

“URA ni timu nzuri wamewafunga Azam na Simba timu ambazo ni nzuri, hivyo tunajiandaa kuhakikisha tunafanya vizuri katika mechi hiyo lengo ni kutwaa ubingwa wa michuano hii na kurejea nyumbani na kombe,”.

Aidha Nsajigwa aliwapongeza vijana wake kwa kujituma mpaka kufikia hatua hiyo, na kuwataka wapambane ili watwae ubingwa huo.

Kwa upande wao Azam kupitia kwa kocha wao msaidizi Idd Cheche wamekiri Singida kuwa timu nzuri na kwamba mchezo huo utakuwa na ushindani mkubwa.

“Singida ni timu nzuri sana na imeleta ushindani mkubwa mno hata kwenye ligi, hivyo tunaamini mchezo huu utakuwa mgumu. Hata hivyo tayari nimewapa maelekezo vijana wangu najua tutashinda tu,” alisema.

Nae kocha mkuu wa Singida Hans Pluijm, alisema mchezo huo utakuwa mkali kwani anaitambua Azam toka akiinoa Yanga, hivyo ni jukumu la wachezaji wake kufanya alichowafundisha.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Clezencia Tryphone

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *