Kitaifa

Nyota 16, majanga yale yale Simba

on

SIKU ya kufa nyani miti yote huteleza…..licha ya kuchezesha nyota 16 katika pambano la leo, kocha Masoud Djuma ameshindwa kuiwezesha timu yake ya Simba kuibuka na ushindi dhidi ya URA.

Simba imekubali kichapo cha bao 1-0 katika mchezo uliomalizika hivi punde kwenye dimba la Amaan hivyo kuondolewa rasmi kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar.

Katika mchezo huo kocha Masoud alifanya mabadiliko mara tano akiwatoa Shiza Kichuya, Jonas Mkude, Nicolas Gyan, Mzamiru Yassin na Mwinyi Kazimoto huku nafasi zao zikichukuliwa na Mohamed Ibrahim, James Kotei, Yusuf Mlipili, Said Ndemla na Laudit Mavugo.

Mabadiliko hayo yalifanya idadi ya nyota waliocheza leo kufikia 16 lakini bado wakishindwa kuikoa timu hiyo kutoka kwenye aibu ya kuondolewa mapema.

Simba ilionekana kumiliki mpira vizuri kipindi cha kwanza
ingawa mipango ya
kutafuta mabao ilikuwa dhaifu hadi kocha huyo alipoanza kufanya mabadiliko ambayo ni wazi hayakuzaa matunda.

Goli pekee katika mchezo huo lilifungwa na Deboss Kalama baada ya kumlamba chenga Erasto Nyoni kabla kupiga shuti lililomshinda kipa wa Simba Emmanuel Mseja.

Simba itarejea jijini Dar es Salaam kuendelea na maandalizi ya mechi za ligi kuu ya Vodacom ambayo wao ndio vinara wakiwa na pointi 26 sawa na Azam.

Mechi nyingine ya kombe la Mapinduzi leo ni kati ya Yanga na Singida United kwenye uwanja huo huo wa Amaan saa 2:15 usiku huu.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *