Afrika

Okwi, Juuko, Niyonzima watemwa Uganda, Rwanda

on

NYOTA wa timu za taifa za Rwanda na Uganda wanaocheza nje ya nchi hizo hawatojumuishwa kwenye vikosi vya CECAFA Senior Challenge Cup baada ya nchi hizo kuomba kutumia wachezaji 23 wanaondaliwa kwa ajili ya michuano ya CHAN nchini Morocco.

Uamuzi huo utawafanya nyota kadhaa wa timu hizo wanaokipiga nje ya nchi wakiwemo Emmanuel Okwi, Juuko Murshid (Uganda, Simba), Haruna Niyonzima (Rwanda, Simba), Michael Rusheshangoga na Danny Usengimana (Rwanda, Singida United) wakose fainali hizo zinazotarajiwa kuanza Disemba 3 mwaka huu.

Uganda na Rwanda zimepata nafasi ya kushiriki fainali cha CHAN hivyo wameona michuano ya Chalenji inaweza kuwasaidia kuandaa vikosi vyao ili wakafanye vema nchini Morocco Januari mwakani.

Timu za taifa za Tanzania, Rwanda, Burundi, Rwanda, Zanzibar, Ethiopia, Libya, Zimbabwe, Sudan Kusini na wenyeji Kenya zitapambana katika michuano hiyo inayotarajiwa kuchukua wiki mbili.

Hii hapa ratiba kamili ya michuano hiyo:

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *