Burudani

One Dance yamuingiza Wizkid kwenye kitabu cha Rekodi cha Guiness

on

MWAKA 2017 unaisha vizuri kwa mwanamuziki wa Afro Pop kutokea Nigeria Ibrahim Balogun maarufu kwa jina la kisanii la Wizkid, amekuwa msanii wa kwanza wa Afro-Pop kuingia kwenye kitabu cha rekodi za dunia ‘Guiness Book of World Records‘ baada ya wimbo wake wa One Dance aliomshirikisha rapa kutoka Marekani Drake kutazamwa mara bilioni moja katika mtandao wa Spotify.

Pia ndani ya mwaka huu Wizkid ameweza kushinda tuzo nyingi kubwa hadi kuwabwaga wasanii wakubwa duniani kama Jay Z.

Zifuatazo ni tuzo alizoshinda Wizkid mwaka huu pekee;


Ghana Music Awards- 02
BET Awards-01
The Headies-05
Nigeria Entertainment Awards-06
MOBO Awards-02
Channe O Music Awards-02
City People Entertainment Awards-02
Dynamix All Youth Awards-02
African Muzik Magazine Awards-02

Jumla ya tuzo alizoshinda ni Tuzo 28 ikiwa ni pamoja na kutajwa katika vipengele 106 vya tuzo tofauti.

Wizkid na Davido wakiwa jukwaani hivi karibuni

Wizkid pia amemaliza tofauti yake na msanii mwenzake wa Nigeria Davido baada ya kupanda jukwaa moja na kuamsha shangwe kubwa kwa mashabiki wao.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *