Kimataifa

Pele atamani kucheza na Ronaldo

on

NGULI wa soka duniani Edson Arantes do Nascimento maarufu kwa jina la Pele ameweka wazi kuwa anatamani angecheza timu moja na nyota wa Ureno na Real Madrid Cristiano Ronaldo enzi zake za kusakata kabumbu.

Pele aliyatoa hayo ya moyoni mara baada ya Ronaldo kutwaa tuzo ya Ballon d’Or ikiwa ni mara ya tano kwa nyota huyo akimaliza 2017 akiwa ametwaa tuzo kadhaa binafsi na zile alizokuwa na Ureno na klabu yake ya Madrid.

Kupitia ukurasa wake wa twitter Pele aliandika “hongera kwa kushinda tuzo ya Ballon d’Or ya mwaka huu, ningependa kucheza upande mmoja na wewe.”

Hii ni mara nyingine nguli huyo anamwagia sifa Ronaldo aliyecheza mechi 882 akipachika mabao 620 huku akitoa pasi za mwisho 202 takwimu zilizompatia matunda ya kutwaa tuzo kadhaa zikiwemo Ballon d’Or tano.

About Abra David Jr

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *