Habari za kuaminika za michezo na burudani kila wakati.

PICHA 5: Samatta alivyoibeba Genk kwa mara nyingine

Safari ya Europa yaanza kunukia

0 481

STRAIKA wa KRC Genk ya Ubelgiji, mtanzania Mbwana Samatta kwa mara nyingine jana aliibeba klabu yake katika kampeni yao ya kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Europa baada ya kuifungia mabao mawili katika ushindi wa 4-1 dhidi ya Charleroi.

Matokeo hayo yameipandisha Genk hadi nafasi ya tano ambapo sasa wanalazimika kushinda mchezo wao wa mwisho dhidi ya Anderletch ili wafuzu kucheza hatua ya Play Off ya Europa
Samatta alifunga mabao yake katika dakika za 24 na 61 huku mengine yakitupiwa nyavuni na Trossard 34′ pamoja na Ndongala 77′
Related Posts
1 of 18
Mkali huyo wa zamani wa African Lyon, Simba SC na TP Mazembe aliifungia goli la kusawazisha timu yake katika mchezo wa katikati ya wiki iliyopita walioambulia sare ya bao moja dhidi ya KAA Gent
Kimahesabu Genk wanahitaji pointi tatu katika mchezo wa mwisho ili washike nafasi ya nne
Msimamo wa Ligi

Get real time updates directly on you device, subscribe now.

Comments
Loading...