Habari za kuaminika za michezo na burudani kila wakati.

PICHA + VIDEO: Simba walivyoivamia Singida alfajiri ya leo

0 1,172

MABASI madogo aina ya Toyota Coaster yasiyopungua matano yameshaingia hapa mjini Singida alfajiri ya leo yakiwa yamejaa mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi Simba waliokuja kuiunga mkono timu yao inayopambana na Singida United leo.

Mara baada ya kuwasili Wanazi hao wa mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom waliangusha ‘kigoma’ cha nguvu ambacho kiliwavuta mashabiki wa Simba waishio mjini hapa waliojiunga kucheza na kuimba nyimbo za kuwakejeli watani zao Yanga.

Mabasi ya mashabiki wa Simba yalipowasili mjini Singida
Related Posts
1 of 18

Taarifa zinadai kuwa mashabiki wengi wa Simba wapo njiani kutokea Dar es Salaam na mikoa ya jirani na Singida wote wakiwa na lengo la kushuhudia pambano hilo la kwanza tangu timu yao itwae ubingwa.

Licha ya kutawazwa mabingwa, Simba wameeleza kuwa hawatopunguza kasi katika michezo yao ili waweke rekodi ya kumaliza ligi bila kupoteza mchezo wowote.

BOIPLUS ipo mjini hapa kukuletea kila kitakachojiri katika pambano hilo linaloonekana kuteka hisia za watu wengi.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.

Comments
Loading...