Burudani

Piga ua wanamuziki hawa watatisha mwaka huu

on

KILA siku kuna wanamuziki wapya na wazuri wanazidi kuongezeka wengine wakiendelea kufanya poa kwa kipindi kirefu lakini baadhi pia wakishindwa kufikia ndoto ama malengo yao.

Mwaka 2017 umeisha ukishuhudiwa gemu la muziki lilivyobadilika na kuwa la ushindani mkubwa kutokana na sasa kuwa ‘muziki biashara’ kwa aslimia mia.

Yapo pia matarajio ya kuwepo kwa ongezeko la wasanii wazuri na watakaotisha sana na kuleta ushindani kwenye soko mwaka huu hasa kutokana na walivyoumaliza mwaka 2017.

Hii hapa ni orodha ya wasanii watano kati ya wengi wa kutazamwa zaidi ama wanaotabiriwa kufanya vizuri zaidi mwaka huu.

1. Lorine Chia-Cameroon


Mwanadada kutoka Cameroon mwenye makazi yake nchini Marekani, akiwa na umri wa miaka 23 tu tayari ameweza kutoa albamu nne.

Licha ya kujaliwa sauti nzuri sana na uwezo mkubwa wa kuimba, Lorine ana uwezo mkubwa wa kucharaza gitaa ambapo alianza kujifunza kutumia chombo hicho akiwa na miaka 15.

Uwezo wake  mkubwa umemfanya apewe shavu na baadhi ya wakali kutoka nchini Marekani kama The Game na Chance the Rapper.

2. Tekno Miles

Ilikuwa ni mwaka 2015 Afrika ilipoanza kumtambua kijana kutoka pande za Nigeria  Augustine Miles Kelechi maarufu kama Tekno akitisha na ngoma ya `Duro’.

Mkali huyo aliendelea kutoa kazi nzuri zilizofanya vizuri kama Pana ambayo imetazamwa katika mtandao wa YouTube kwa takribani mara 20 milioni.

Wimbo huo ulimpatia mafanikio makubwa sana ikiwa ni pamoja na kusaini bonge la dili na lebo kubwa ya kurekodi nyimbo duniani kutoka Marekani Columbia Records akiungana na wakali kama John Legend na Pharrell William.

3. Vanesaa Mdee

Huyu ni Vee Money mkali wa kibao cha `Bounce’ kutoka Mdee Music tangu ajitambulishe rasmi kwenye ‘game’ mpaka sasa ameendelea kudhihirisha kuwa muziki ni kipaji chake toka moyoni kwani hajawahi kushuka kimziki.

Ngoma kama Niroge, Cash Madame, Kisela ni kati ya kazi zake zilizofanya vizuri sana.

2018 anategemewa kufanya makubwa zaidi huku akiwa anajiandaa kuzindua albamu yake kwa jina la `Money Monday’ ambayo amewashirikisha nyota kibao kama Joh Makini kutokea Weusi, Mohombi, Casper Nyovest na wengine wengi.

4. Frank Casino

Afrika kusini ni moja ya nchi zinazofanya vizuri sana katika muziki wa Hip Hop, huku ikishuhudiwa wakali kama AKA na Casper Nyovest wakifanya vizuri sana.

Leo tunakuletea kijana mwingine kutokea kwa Zulu au kwa Madiba Frank Casino ambaye ni rapa anayekuja huku akitegemewa kufanya vizuri zaidi mwaka huu.

5. Phy 

Mzaliwa wa jiji la Nairobi nchini Kenya namleta kwenu Phy, huyu alikuwa mshindi wa msimu wa kwanza kabisa wa mashindano ya kutafuta vipaji vya muziki Afrika Mashariki yanayojulikana kama `Maisha SuperStar’ mwaka 2015.

Baada ya kushinda alifanikiwa kutoa albamu yake kwa jina `Philosophy’ na kutajwa kama mwanamuziki kijana mwenye kipaji cha aina yake. Jinsi alivyoumaliza mwa ka 2017 ni ishara tosha ya yeye kufanya vema zaidi mwaka huu.

Usiache kutembelea kwenye mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Instagram na Twitter kwa jina la BOIPLUS MEDIA na pia SUBSCRIBE kwenye chaneli yetu YouTube (BOIPLUSTV) kwa kubonyeza picha hii hapa chini;

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *