Kitaifa

Polisi wavunja mkutano Yanga

on

JESHI la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, limezuia mkutano wa wanachama na viongozi wa matawi wa Yanga uliotarajiwa kufanyika leo makao makuu ya klabu hiyo.

Jeshi hilo limefikia hatua hiyo baada ya kubaini kupitia kwa OCD Ibrahim aliyefikia hatua ya kuupiga ‘stop’ mkutano huo kutokana na viashilia vya uvunjifu wa amani.

“Tumeafikiana kikao cha leo kisifanyike, na hiyo ni kutokana na uvunjifu wa amani kwa taarifa tulizozipata, hivyo baada ya kujiridhisha uwepo wa mkutano huo tutawaruhusu wafanye chini ya uangalizi wetu,” alisema.

Kabla ya askari kuzuia mkutano huo wanachama wa klabu ya Yanga walikuwa wameishafika klabuni hapo tayari kwa ajili ya kuanza mkutano uliokuwa na lengo la kujadili mambo mbalimbali yahusuyo klabu hiyo.

“Askari walikuwa wengi bila sababu za msingi sisi tunajadiliana mambo ya manufaa na kinachoendelea Yanga, wao wanatukatalia kufanya mkutano wetu ambao una amani, mfano mimi nimetoka Zanzibar kwa ajili ya mkutano,” alisema mwanachama aliyejitambulisha kwa jina la Said.

Kwa upande wake Bakili Makele alimtuhumu katibu wa Wazee Ibrahim Akilimali kuwa ndio chanzo cha migogoro ndani ya klabu yao.

Alisema Akilimali na wenzake wanapita sehemu mbalimbali kwenye maofisi ya watu na kuipakazia Yanga maneno yasiyo rasmi.

Aidha Makele alisema wanatambua hali ndani ya Yanga kiuchumi lakini wanaushukuru uongozi wao kwa kuiandaa timu ambayo iko katika msimamo mzuri sana kwa sasa.

“Mpaka sasa kuna wenzetu wako Polisi wanaweka mambo sawa tuna imani wataturuhusu tu kufanya mkutano wetu, kwani Polisi ni watu wa kulinda amani hivyo baada ya kujiridhisha watatupa nafasi tujadili yetu,”alisema Makele.

Aliongeza kwa kuwataka wanayanga kote waliko wawe na amani kwani hakuna mgogoro wowote ndani ya timu zaidi ya Akilimali na wenzake wachache kuichafua huko wapitako.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Clezencia Tryphone

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *