Kimataifa

PSG waamua kuibomoa Madrid ili kumfurahisha Neymar

on

PSG wameshtuka kwamba kuna uwezekano Real Madrid wakafanikiwa kuinasa saini ya nyota wao Neymar Jr kwavile mbrazili huyo hana furaha na straika mwenzake Edinson Cavan tangu wagombee penati.

Unajua walichowaza haraka haraka?, ni kumuuza Cavani na kumsajili Karim Benzema ambaye wanaamini yeye na Kylie Mbappe watakubali kukaa chini ya kivuli cha Neymar tofauti na raia huyo wa Uruguay ambaye amekuwa ‘akimvimbia’.

Neymar aliyetupia mabao 24 katika michezo 23 tu chini ya kocha Unai Emery alitua klabuni hapo akitokea Barcelona kwa ada ya uhamisho ya paundi 200 milioni iliyovunja rekodi ya dunia baada ya mbrazili huyo kununua mkataba wake.

Karim Benzema

Kwa mujibu wa Don Balon, Rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi anajiandaa kumruhusu Neymar azungumze na Madrid endapo tu ataiwezesha timu hiyo kutwaa taji la ligi ya mabingwa Ulaya lakini tofauti na hapo atafanya kila liwezekanalo kumfurahisha nyota huyo ili aendelee kuwepo kikosini hapo.

PSG wapo tayari kuilipa Madrid paundi 52.3 milioni (Euro 60 milioni) ili kumng’oa Benzema Santiago Bernabeu ambapo amekuwa na msimu mgumu na mabingwa hao wa Ulaya wapo tayari kumuuza majira ya joto.

Taarifa kutoka Hispania zinadai Arsenal pia wanamtaka Benzema ili kukiongezea nguvu kikosi chao baada ya kuondoka kwa straika wao Alexis Sanchez aliyetua Manchester United.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *