Habari za kuaminika za michezo na burudani kila wakati.

RASMI: Simba washangilia ubingwa kwenye basi wakielekea Singida

0 1,294

HATIMAYE imewezekana….
Klabu ya Simba ni mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom wakitwaa taji hilo la msimu wa 2017/18 wakiwa ndani ya basi kuelekea Singida hiyo ikiwa ni baada ya Yanga kufungwa mabao 2-0 na Prisons ya jijini Mbeya.

Matokeo hayo ya Yanga iliyobaki na pointi zake 48 yanamaanisha wakishinda mechi zao tano zilizobaki watafikisha pointi 63 tu ambazo Simba wenye pointi 65 walishazipita.

Simba wamekuwa kwenye kiwango bora msimu huu ambapo wameongoza ligi kwa kipindi kirefu na sasa wanatangaza ubingwa wakiwa na mechi tatu mkononi.

Related Posts
1 of 18
Simba mabingwa 2017/18

Wekundu hao wa Msimbazi watawasili jijini Dodoma leo ambapo watalala na kukutana na wabunge mashabiki wa timu hiyo kabla hawajaendelea na safari kesho kuifuata Singida United watakaopambana nao keshokutwa Jumamosi kwenye dimba la Namfua.

Simba imetwaa ubingwa huo ikiwa ni baada ya misimu mitano kupita wakiambulia patupu tangu watwae ‘ndoo’ msimu wa 2011/12.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.

Comments
Loading...