Burudani

Ray C ‘kutoka’ na Yemi Alade mwaka huu

on

MWANADADA mkongwe katika tasnia ya muziki wa bongo fleva hapa nchini, Rehema Chalamila ‘Ray C’ anawaza kutoka na mwanamuzi wa Nigeria, Yemi Alade.

Ray C aliyetamba na nyimbo zake kama ‘Uko Wapi’, ‘Milele’, ‘Mahaba ya dhati’ na nyingine kadhaa aliwahi kujipatia umaarufu kutokana na uwezo mkubwa wa kucheza stejini mpaka kupachikwa jina la ‘kiuno bila mfupa’.

Posti ya Ray C katika mtandao wa Instagram

 

Kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram msanii huyu aliweka picha ya ‘posti’ iliyowekwa na mtandao wa ATMUZIK walioonyesha kutamani kuona nyota huyo akitoa ngoma na Yemi Alade na yeye kukubali wazo hilo kwa kusema “Your wish is my command” akimaanisha “ombi lenu ni amri kwangu,”.

Posti hiyo ya Ray C aliye kimya kwa kipindi kirefu ni dalili kwamba nyota huyo anaweza kuanza michakato ya kufanya kazi na mnaijeria huyo.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Isaya Mwaseba

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *