Kimataifa

Ronaldo asawazisha dakika ya mwisho Ballon d’Or

on

‘PAMBANO’ kali la miaka 10 ya kuwania tuzo ya mchezaji bora wa dunia (Ballon d’Or) kati ya Cristiano Ronaldo na Lionel Messi limemalizika muda mfupi uliopita ikishuhudiwa nahodha huyo wa Ureno akisawazisha ‘dakika’ ya mwisho.

Ronaldo ametwaa tuzo hiyo usiku wa Alhamisi akimbwaga mpinzani wake mkuu Messi lakini ni kwamba amesawazisha tu, hajaibuka bingwa.

Unakumbuka?
Kwa miaka 10 sasa hakuna mchezaji mwingine yeyote aliyewahi kutwaa tuzo hiyo yenye heshima kubwa duniani mbali ya Ronaldo na Messi, lakini cha kustaajabisha ni kwamba wakali hao wamepiga ‘pasu’.

Kabla ya tuzo ya leo Ronaldo alikuwa ametwaa mara nne tangu 2008 huku Messi akiwa na tano kabatini kwake, hivyo straika huyo wa Real Madrid ni kama vile amesawazisha dakika ya mwisho wakati miaka yao 10 ikiwa inamalizika usiku huu.

Messi alitwaa tuzo hiyo 2009, 2010, 2011, 2012 na 2015 huku Ronaldo akitwaa 2008, 2013, 2014, 2016 na 2017.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *