Burudani

Ruby katoa somo la ‘kiki’ mpya mjini

on

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini  Hellen George ‘Ruby’ ameonyesha kukerwa na mastaa wa kike wanaotafuta ‘kiki’ kwa kukaa nusu uchi na badala yake ametaka wawe wabunifu.

Ruby aliyefanya vizuri katika ‘game’ na kibao chake cha ‘na yule’ alizua gumzo katika mitandao ya kijamii baada ya kuweka picha zilizomuonyesha kaongeza maumbile yake.

Hii ndio picha ya kuhaririwa aliyoipost Ruby

Kitendo hicho cha msanii huyo amesema kilitokana na yeye kukerwa na tabia ya wasanii wengi wa like kutafuta kiki kwa kuposti picha za nusu utupu akidai amefanya hivyo kuwapa somo mastaa wengine.

Ruby alisema ili kupata umaarufu katika mitandao si lazima uweke picha zisizo na maadili bali unaweza kufanya ubunifu kama alioufanya yeye.

Msanii huyo alifunguka hayo akiwa katika mahojiano na kituo cha televisheni cha EATV.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Isaya Mwaseba

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *