Kimataifa

Sikia alichosema ‘Ustadh’ Salah kuhusu ubingwa Liverpool

on

LIVERPOOL haijawahi kubeba ubingwa tangu 2012 walipotwaa kombe la ligi chini ya kocha Kenny Dalglish, lakini Mohamed Salah anaamini msimu huu hawatoki kapa, lazima wataambulia chochote.

Mshambuliaji huyo amekuwa katika kiwango cha juu tangu atue kwa Majogoo hao akitokea Roma hali inayopelekea mashabiki wa timu hiyo waamini atamaliza ukame wa vikombe klabuni hapo.

Ligi ya mabingwa na kombe la FA ndio makombe pekee ambayo Liverpool naweza kubeba msimu huu hivyo imani ya Salah itakuwa imelala katika moja ya vikombe hivyo.

“Siku zote nasema nahitaji kubeba mataji hapa, nimekuja hapa kushinda chochote tu kwa ajili ya klabu hii, kwa ajili yetu wachezaji na kwa ajili ya mashabiki wetu,” Salah aliiambia Sky Sports News.

Raia huyo wa Misri aliyetupia mabao 21 katika mechi 27 aliongeza kuwa wachezaji wa timu hiyo wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii siku zote ili kupata kombe msimu huu.

Katika magoli hayo 21, magoli 15 ameyafunga kwenye ligi kuu ikiwa ni idadi sawa na aliyotupia Harry Kane wakibanana kileleni mwa orodha ya wafungaji hadi sasa.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *