Makala

Siku nyingine mkumbusheni Tshabalala ‘kumheshimu’ nahodha

on

NDIO….wakati mwingine inatokea mtu unafanya kitu cha ajabu kabisa kwavile tu kuna jambo hujalikumbuka, binadamu tumeumbiwa kusahau lakini madhara ya ulichokifanya yatabaki pale pale.

Hili ndilo lililotokea katika mchezo wa kombe la Mapinduzi kati ya Simba na Mwenge pale nahodha wa Wekundu hao alipoingia kuchukua nafasi ya kinda Moses Kitandu, nahodha msaidizi Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ akasahau kufanya kitu kikubwa sana.

Kwa heshima na inavyofanyika maeneo mengi dunianu ni kwamba inapotokea nahodha anaanzia benchi huku msaidizi akivaa kitambaa cha unahodha, basi akiingia ni lazima arejeshewe kitambaa chake mara moja.

Hii ni tofauti kabisa na kilichotokea katika mchezo wa leo ambapo Tshabalala aliendelea kubaki na kitambaa hicho hadi mechi ilipomalizika. Sitaki kuamini kuwa beki huyo wa kushoto halijui jambo hilo, bali alisahau.

Viongozi wa benchi la ufundi ama wachezaji wenzake walipaswa kumkumbusha juu ya jambo hilo muhimu na la kistaarabu. Isingekuwa rahisi kwa Bocco kumfuata Tshabalala na kumuomba kitambaa hicho.

Method Mwanjali (kushoto) akiwa na Tshabalala katika utambulisho wa jezi mwanzoni mwa msimu huu

Baada ya kuondoka kwa Method Mwanjali, aliyekuwa msaidizi wake namba (Bocco) amekuwa ndiye nahodha mkuu huku akisaidiwa na Tshabalala.

 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Karim Boimanda

Recommended for you

1 Comment

  1. Hamid

    January 2, 2018 at 9:47 pm

    Tshabalala ndiye alikuwa nahodha namba mbili wa Mwanjali, Bocco namba tatu, hivyo hakuna kosa alilofanya labda kama kuna mabadiliko yalifanywa baada ya kuondoka Mwanjali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *