Kitaifa

Simba kutua Shinyanga bila Kwasi

on

KIKOSI cha Wekundu wa Msimbazi Simba kinatarajia kuondoka alfajiri ya Jumanne kwa usafiri wa anga kuelekea mjini Shinyanga kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mwadui FC huku nyota wake Asante Kwasi akibakia jijini Dar akitumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

Kwasi aliyesajiliwa na Simba katika dirisha dogo lililopita na kufanikiwa kuingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza ameachwa kwenye msafara huo wa wachezaji 20 kutokana na kadi tatu hizo ambazo mbili alizipata akiwa Lipuli FC na nyingine Simba.

Wachezaji wanaosafiri ni
Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Emanuel Mseja, Aishi Manula, Laudit Mavugo, Mzamiru Yassin, John Bocco, Mwinyi Kazimoto, Said Hamis, Nicholas Gyan, Moses Kitandu na Ally Shomari.

Wengine ni Juuko Murshid, James Kotei, Yusufu Mlipili, Mohamed Hussein, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Emmanuel Okwi na
Paul Bukaba.

Simba itacheza na Mwadui Alhamisi ya Februari 15 na itarejea jijini Dar es Salaam siku ya pili yake kabla ya kuondoka Februari 18 kuelekea nchini Djibout kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gendarmerie Nationale.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Akram Msangi

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *