Makala

Simba mmeghairi kulea ‘watoto’?

on

KUNA watu wanaacha mabaya na kuanza kutenda mema, hawa huwa hawazungumzwi sana kwavile inaonekana ni kama vile
wametimiza wajibu wao, lakini wapo wanaoacha mema na kuanza
kufanya mabaya, hawa hawawezi kukwepa kelele zetu sisi ‘wazee wa
gubu’.

Hii haijaanza leo, hata tukiwa wadogo wazazi wetu walikuwa wazito
sana kutusifia waziwazi pale tunapofanya vema, lakini usiombe
ukosee, mtaa mzima utapata taarifa.
Asubuhi ya leo kimetangazwa kikosi cha wachezaji 35 watakaounda
timu ya taifa ya Tanzania chini ya miaka 23 (U23) wakitokea katika
timu 17 tofauti ikiwemo Simba SC ya jijini Dar es Salaam.

Kilichonishtua katika kikosi hiki ni kitendo cha Wekundu hao kuwa
na mchezaji mmoja tu, Yusuph Mlipili ambaye amesajiliwa msimu huu
akitokea TotoAfrican ya jijini Mwanza.
Sijashtuka kwa sababu ya ukubwa wa jina la Simba, hapana, bali
kutokana na ninavyofahamu ubora wa Simba linapokuja suala la
kukuza na kulea vipaji vya vijana, kwanini leo wawe na mchezaji
mmoja tu tena ambaye wala hajatokea kwenye kikosi chao cha
vijana?.

William Lucian ‘Gallas’ wa Ndanda FC (kushoto) akipambana na Ibrahim Ajib wa Yanga. Wote hawa ni mazao ya Simba B

Wachezaji wengi sana wanaozitumikia timu za ligi kuu ya Vodacom
wamepitia kwenye timu ya vijana ya Simba hii ni kuthibisha hiki
nikisemacho kuwa hawa jamaa wanatisha kwenye sekta hiyo, lakini
nini kimewapata?, Simba mmeghairi kulea vijana au mnaelea ambao
hawana ubora kama wa akina Ibrahim Ajib?
Sitaki kuamini sasa timu ya vijana ya Simba haijatoa hata mchezaji
mmoja wa timu ya taifa (U23), si hali ya kawaida, sifa ile iliyoletwa na
akina Patrick Rweyemamu(kocha) imepotezwa na nini?

Naamini uongozi uliopo madarakani hautochukulia suala hili kama
jambo la kawaida kwavile ni dalili mbaya, hata timu zenye utajiri
mkubwa kama Real Madrid bado zinakuza vijana wenye vipaji ambao
huwapandisha kikosi chao cha kwanza na wengine wakiuzwa kwenye
klabu zingine.

Kikosi cha timu ya taifa (U23) kilichotangazwa leo

Kikosi cha vijana cha Simba maarufu kama Simba B kilichokuwa
kikiundwa na wachezaji kama Jonas Mkude, Said Ndemla, Ajib,
Hassan Isihaka, Abdallah Seseme, William Lucian ‘Gallas’,
Edward Christopher, Miraji Adam na wengine wengi kilikuwa
kikionesha wazi dalili za kuzalisha nyota wengi tofauti na hiki cha
sasa ambacho wachezaji wengi wanaonekana ni wa kawaida sana.

Azam FC imetoa vijana watano katika kikosi hicho cha timu ya
taifa (U23) huku Yanga ikitoa wanne. Timu za Mtibwa Sugar,
Mbeya Cityna na Ndanda FC zimetoa wachezaji watatu kila moja
wakati Prisons, Majimaji FC, Stand United, Njombe Mji na
Singida United zikitoa wachezaji wawili kila moja.

Timu zilizotoa mchezaji mmoja ni Ruvu Shooting, JKT Ruvu,
Ashanti United, Mwadui FC, Miembeni, JKU na Simba SC.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *