Habari za kuaminika za michezo na burudani kila wakati.

SINGIDA: Namfua si mahala pa kutangazia ubingwa, ni kisasi tu kwa Simba

0 817

KOCHA msaidizi wa Singida United Jumanne Chale amewahakikishia pointi tatu mashabiki wa timu hiyo katika mchezo wa Jumamosi hii dhidi ya Simba huku akisisitiza ni mechi ya kisasi.

Kocha huyo amesema Simba wasitarajie mteremko katika mchezo huo na kutangaza ubingwa kwenye uwanja wa Namfua kwavile wao wanataka kulipa kisasi cha kichapo cha mabao 4-0 walichopokea jijini Dar es Salaam.

“Tulipomaliza tu mechi iliyopita tulianza hapo hapo maandalizi ya mechi dhidi ya Simba. Tunaichukulia kwa uzito mkubwa kwa sababu tunaiheshimu ni timu kubwa na ilitufunga 4-0 lakini bado tunataka kuendeleza rekodi yetu ya kutofungwa nyumbani.

Related Posts
1 of 18
Tafadzwa Kutinyu ataikosa Simba Jumamosi hii. PHOTO: Singida United

“Wana wachezaji wazuri lakini sisi pia tuko vizuri kwa maana hiyo Jumamosi sio siku ya Simba kutangaza ubingwa kwenye Uwanja wetu wa nyumbani. Watambue hii mechi ni ngumu mno na pia ni mechi yetu ya kulipiza kisasi,” Alisema Jumanne.

Singida ambayo ipo nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi itawakosa wachezaji wake wawili muhimu ambao ni Tafadzwa Kutinyu mwenye kadi tatu za njano na Michael Rusheshangoga ambaye ana matatizo ya kifamilia.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.

Comments
Loading...