Boiplus

SportPesa Waamua Kuwachonganisha ‘Watu’ Wao

on

KAMPUNI ya SportPesa inayokuja kwa kasi katika tasnia ya soka Tanzania imeanzisha michuano itakayozikutanisha timu nane inazozidhamini kutoka Tanzania na Kenya.

Kwa hapa nchini SportPesa itaanza kuzidhamini kuanzia msimu mpya wa ligi 2017/18 timu za Simba, Yanga na Singida United huku Jang’ombe Boys kutoka visiwani Zanzibar ikijumuishwa pia kwenye michuano hiyo.

Michuano hiyo itakayoanza Juni 4 hadi 11 hapa jijini Dar es Salaam itakuwa na makundi mawili ambapo pia timu za Tusker FC, Gor Mahia, Nakuru All Stars na AFC Leopards kutoka Kenya zikitarajiwa kushiriki.

Katika michuano hiyo huenda miamba ya soka nchini timu za Simba na Yanga zikakutana kama zitafanikiwa kutinga fainali kwakua kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa timu hizo hazitakuna katika hatua nyingine.

Bingwa wa michuano hiyo atanyakua kitita cha dola 30,000 huku mshindi wa pili akipata dola 10,000 na timu shiriki zikipata milioni 5 kila moja kama kifuta jasho.

Ratiba kamili ya michuano hiyo ni kama ifuatavyo:

Juni 4
Singida Utd v AFC Leopards
Yanga v Tusker

Juni 5
Simba v Nakuru
Jang’ombe Boys v Gor Mahia

Nusu Fainali 1 Juni 7

Nusu fainali 2 Juni 8

Fainali Juni 11

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *