Kitaifa

Taarifa kamili kuhusu afya ya Aveva Muhimbili

on

HALI ya Rais wa Klabu ya Simba Evance Aveva inaendelea kuimarika baada ya jana kukimbizwa katika hospitali ya taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Aveva na makamu wake Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ wapo mahabusu katika gereza la Keko toka mwaka jana, wakituhumiwa kwa kosa la utakatishaji fedha.

Akizungumza na BOIPLUS leo, msemaji wa Hospitali ya Muhimbili Neema Mwangomo alikiri Aveva kupokelewa katika hospitali hiyo majira ya saa 4 usiku baada ya kuugua ghafla akiwa gerezani Keko.

Neema alisema, hali ya mgonjwa inaimarika kwa sasa tofauti na alivyofikishwa jana hata hivyo anendelea na matibabu zaidi.

“Jana saa 4 usiku aliletwa hapa, ila kwa sasa anaendelea vizuri sana, amepumzishwa Sewahaji namba 18, tunaimani atapona tu,” alisema na kuongeza kuwa kujua anaumwa nini ni siri yake na daktari wake anayemtibu.

Habari ambazo BOIPLUS ilizipata jana kutoka kwa mtu wa karibu wa kiongozi huyo, zinasema kabla ya kupelekwa Muhimbili alitolewa Hospitali ya Temeke baada ya kuona hali yake hairidhishi.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Clezencia Tryphone

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *