Burudani

TOP TEN: Video za muziki zilizotazamwa mara nyingi zaidi Youtube ndani ya masaa 24

on

Kuna njia nyingi za kupima mafanikio ya kazi uliyoifanya na kuweza kujua nini hatma yako mbeleni.

Kukua kwa teknolojia kumerahisisha sana kazi za sanaa, kwa kipindi cha hivi karibuni wasanii wa muziki wamekuwa wakitumia mitandao kufikisha kazi zao sehemu tofauti duniani na kuwaongezea mashabiki pia kuongeza kipato chao.

Mtandao unaotumiwa zaidi na wasanii ni YouTube ambapo wanamuziki wanaweza kujitathmini kwa kuona idadi ya watu waliotazama video zao, kwa Tanzania tumeona wasanii Diamond Platnumz na Ali kiba wao ndo wanaongoza kwa kazi zao kutazamwa sana Youtube.

Kutambua hilo BOIPLUS tumekuletea video 10 zilizotazamwa mara nyingi ndani ya masaa 24 tangu ziwekwe katika mtandao huo.

1. Look What You Made Me-Taylor Swift video hii ilitazamwa mara 43.2 milioni ndani ya masaa 24

 

2.Gentlemen-Psy

Ilitazamwa mara 38.4 milioni

 

3.Hello-Adele

Wimbo huu umerudiwa na watu wengi zaidi, video ilitazamwa mara 27.7 milioni ndani ya masaa 24.

 

4.Suara Cara-Major Lazer Ft Anitta & Pabllo Vittar

Video ilitazamwa mara  25 milioni ndani ya masaa 24

 

5. Despacito(Remix)-Luis Fonsi, Daddy Yankee ft Juatin Beiber

Video hii inakamata nafasi ya tano baada ya kutazamwa mara 23.7 milioni ndani ya masaa 24

6. Boom Boom- Daddy Yankee Ft Redone, French Montana & Dinah Jane

Ipo nafasi ya sita, ilitazamwa mara 23 milioni ndani ya saa 24.

 

7.DNA-BTS

Moja kati ya video zilizowapagawisha watu. Hii ilitazamwa mara 21 milioni masaa tu tangu itupiwe YouTube.

 

8. Ready for it- Taylor Swift Ft Kendrick Lamar

Video hii ilitazamwa mara 20.1 milioni ndani ya saa 24

 

9.Anaconda- Nicki Minaj

Nicki Minaji amekata nafasi ya tisa baada ya video yake ya Anacond ambayo ilizungumzwa sana, kutazamwa mara 19.6 milioni ndani ya masaa 24.

 

10. Nafasi ya Kumi imeshikwa na mwanadada Miley Cyrus na Kibao chake cha Wrecking Ball.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *