Kitaifa

Treni imekolea moto, Yanga yakamata tisa nje

on

KAMA masihara vile, mabingwa watetezi Yanga wameonyesha wanaendelea ‘kunoga’ baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Lipuli FC kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa jioni ya leo.

Huu unakuwa ni ushindi wao wa tatu mfululizo kwenye ligi kuu ya Vodacom ambapo wamefanikiwa kujikusanyia jumla ya pointi tisa katika mechi hizo ambazo zote ni za ugenini.

Mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo haukuwa mzuri kwa Yanga hasa walipocheza nyumbani huku pia wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kuchapwa mabao 2-0 na Mbao FC jijini Mwanza Disemba 31.

Baada ya kupoteza mchezo huo dhidi ya Mbao, Januari 17 Yanga walilazimishwa sare tasa na Mwadui jijini Dar es Salaam hayo yakiwa ndio matokeo ya mwisho kuwahuzunisha mashabiki wao.

Yanga waliibuka na ushindi wa bao moja dhidi ya JKT Ruvu kabla ya kuibutua Azam FC mabao 2-1 Chamazi na leo wakishinda mchezo wao wa tatu ugenini dhidi ya Lipuli.

Mabao yaliyowanyamazisha wanazi wa Lipuli katika mchezo huo yaliwekwa nyavuni na Papy Tshishimbi pamoja na Pius Buswita.

Matokeo ya mechi nyingine za leo ni kama ifuatavyo;
Singida United 3-2 Mwadui FC
Majimaji FC 1-2 Mbeya City
Prisons 2-0 Njombe Mji

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *