Kimataifa

ULISIKIA HII?: Kilinuka vyumbani baada ya Mourinho kuwalazimisha City wapunguze kelele za kushangilia

on

KAMA ulidhani wewe shabiki wa Manchester United umevurugwa sana na matokeo ya jana basi tambua kocha Jose Mourinho amevurugwa zaidi yako.

Mabao ya David Silva na Nicolas Otamendi yaliufanya uwanja wa Old Trafford uzizime kwa majonzi huku zikisikia sauti za mashabiki na wachezaji wa Manchester City wakishangilia ushindi wao.

Ishu ilikuaje?
Baada ya kumalizika kwa mchezo huo wachezaji wa City waliingia chumbani kwao na kuanza kuimba na kushangilia kwa sauti ya juu kutokana na ushindi huo wa ugenini katika ‘derby’ ya jiji la Manchester.

Wakati huo hayo yanaendelea hali ya Mourinho ilionekana kuwa si ya kawaida akionesha hasira za wazi ndipo aliposhindwa kuendelea kuvumilia kelele hizo.

Kama mbwai mbwai tu
Mourinho si akajitosa chumbani kwa City bwana, bila kupepesa macho akawaambia “Punguzeni kidogo sauti zenu na muoneshe heshima kwa United”.

Kauli hiyo ya Mourinho ni kama vile iliamsha zaidi kelele huku likizuka zogo kubwa kati ya kocha huyo na wachezaji waliokuwa wakiendelea kushangilia.

Ederson akanunua ugomvi
Licha ya wachezaji wengine kuonesha kutofurahishwa na kauli ya Mourinho, kipa mbrazili wa City, Ederson alimvaa kocha huyo mwenye maneno mengi na kuanza kurushiana naye maneno kwa lugha ya kireno.

Hatari tupu
Usidhani zogo liliishia kwenye maneno tu, katika mgogoro huo ambao baadae uliingiliwa na wachezaji wa timu zote, Mourinho alipigwa na chupa ya maji kichwani huku ‘tifu’ likimuacha nyota wa zamani wa Arsenal aliye kwenye benchi la ufundi la City, Mikel Arteta akivuja damu.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *