Burudani

Unamkumbuka Bizman?, yupo zake Ujerumani anapiga kazi kama kawa

on

MSANII aliyetamba miaka iliyopita na ngoma yake ya ‘Ametoroshwa’ Emmanuel Ntavyo ‘Bizman’ amesema, ziara yake nchini Ujerumani itazidi kumfanya awaze kutoa vitu vipya.

Akizungumza na BOIPLUS leo akiwa Ujerumani, Bizman ambaye anayemiliki bendi yake ya Inafrika alisema, ziara yao hiyo ni kwa ajili ya kutoa burudani murua katika maeneo mbalimbali nchini humo huku wakitarajia kukaa nchini humo miezi miwili na baadae kurejea hapa nchini na kuendelea na majukumu yao.

Inafrika Band wakiwa nchini Ujerumani

“Inafrika tunatembelea nchi mbalimbali kwa ajili ya kufanya shoo, na tuna wapenzi wetu wengi kwani sio mara ya kwanza kuja,”alisema.

Inafrika inanyimbo mbalimbali zikiwemo Indege, Julie, Mgema, Omunwa, Mulelwa, Wazazi na Ngoma zetu.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *