Kitaifa

Unamzuiaje Zimbwe Jr Kutwaa Tuzo?

on

BAADA ya kuitumia Simba katika michezo yote ya ligi kuu tena kwa kiwango cha hali ya juu, hakukuwa na uwezekano wa kumzuia beki wa kushoto wa timu ya Simba Mohammed Hussein ‘Zimbwe Jr’ kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa ligi msimu wa 2016/17 katika hafla za utoaji tuzo zilizofanyika jana kwenye ukumbi wa Mlimani City.

Zimbwe ambaye alicheza mechi hizo zote za ligi bila kufanyiwa mabadiliko alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda Aishi Manula mlinda mlango wa Azam FC na kiungo mshambuliaji wa mwenye kasi wa Yanga Simon Msuva.

Mchezaji mwingine wa Simba Shiza Kichuya alipata tuzo ya bao bora alilofunga dhidi ya Yanga Februari 25 alilofunga akiwa nje ya 18 baada ya kuwatoka walinzi wa Yanga na kuipa Simba bao la ushindi.

Bao hilo la Kichuya limechaguliwa baada ya kuyashinda mabao mengine mawili yaliyofungwa na Peter Mwalyanzi anayecheza kwa mkopo African Lyon akitokea Simba na Zahoro Pazi wa Mbeya City aliyefunga dhidi ya Mbao FC.

Mbaraka Yusuf wa Kagera Sugar amechaguliwa kuwa mchezaji bora chipukizi katika msimu ambao umemalizika Jumamosi iliyopita.

Mbaraka ameshinda tuzo hiyo huku akiwa miongoni mwa wachezaji waliofunga zaidi ya mabao 10 katika msimu huo.

Kipa namba moja wa Azam FC, Aishi Manula ametangazwa kuwa kipa bora licha ya timu yake kumaliza nafasi ya nne kutokana na kutokuwa kwenye ubora mzuri msimu uliopita.

Kiungo wa Yanga Haruna Niyonzima amefanikiwa kutwaa tuzo ya mwanasoka bora wa ligi kuu kwa wachezaji wa kigeni.

Niyonzima ameisaidia Yanga kutwaa ubingwa wa ligi kuu mara ya tatu mfululizo akitoa msaada mkubwa kwa timu hasa mzunguko wa pili alipoanza kupewa nafasi zaidi kikosini.

Kocha wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amechaguliwa kuwa kocha bora wa msimu wa 2016/17 kutokana na ubora mkubwa aliyoonyesha tangu ajiunge na timu hiyo akitokea Mtibwa Sugar.
KIKOSI BORA CHA MSIMU 2016/17

1. Aishi Manula – Azam FC

2. Salum Kimenya – Prisons

3. Mohamed Hussein – Simba

4. Mohamed Yakubu-Azam

5. Method Mwanjale – Simba

6. Kenny Ally- Mbeya City

7. Simon Msuva-Yanga

8. Haruna Niyonzima – Yanga

9. Abdulrahman Musa – Ruvu Shooting

10. Mbaraka Yusuf – Kagera

11. Shiza Kichuya – Simba

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *