Kimataifa

United Watwaa Europa kwa Mara ya Kwanza

on

STOCKHOLM, Sweden
MANCHESTER United ya Jose Mourinho imeweka historia ya kutwaa taji la Europa kwa mara ya kwanza baada ya kuifunga Ajax Amsterdam mabao 2-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika kwenye uwanja Friends Arena jijini Stockholm, Sweden.

Mabao ya Paul Pogba na Henrikh Mkhtaryan yalitosha kuipa United ubingwa huo licha ya Ajax kumiliki mpira zaidi katika muda mwingi wa mchezo huo.

Ubingwa huo unamfanya kocha Jose Mourinho kuandika historia ya kutwaa mataji yote makubwa katika ngazi ya klabu.

Ajax ambayo inaundwa na wachezaji wengi vijana itabidi wajilaumu wenyewe kwa kutengeneza nafasi nyingi za kufunga na kumiliki mpira lakini wakashindwa kupata mabao.

United ilimaliza nafasi ya sita katika msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza hivyo ubingwa huo umekuwa faraja pekee kwa wapenzi na mashabiki wa Mashetani hao wa Old Trafford.

Ubingwa huo unaipa United tiketi ya moja kwa moja ya kushiriki ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya msimu ujao baada ya msimu uliopita kushindwa kushiriki.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *