Kimataifa

Utetezi wa Binti wa Figo kuhusu video ‘zake’ chafu

on

BINTI wa nyota wa zamani wa Real Madrid na Barcelona, Luis Figo amekanusha vikali madai ya kuhusika katika video ya ngono iliyosambazwa kwenye mitandao mbalimbali akisisitiza amefanana tu na binti aliyejirekodi.

Mapema wiki hii kulikuwa na video inayosambazwa ikimuonyesha Daniela Figo, 18, akifanya mapenzi hali iliyopelekea mrembo huyo avunje ukimya na kufunguka kuwa ni mtu aliyejifananisha na yeye ili kumchafua tu.

Daniela aliandika kwenye akaunti yake ya mtandao wa Instagram akiwaeleza mashabiki wake zaidi ya 13,000 maelezo marefu yaliyoonekana kuwa katika mlengo wa utetezi.

Daniela Figo

“Hivi karibuni kumekuwa na picha na video mbaya zinazosambaa katika mitandao ya Instagram na Whatsapp zikimuonyesha binti anayejifananisha na mimi.

“Napenda mfahamu kuwa picha na video hizo si zangu. Kiukweli sielewi nini hasa lengo lake na inasikitisha sana kuona baadhi ya watu wanapenda kutunga mambo ya uongo kupitia picha na video za mtu ambaye hata hawamfahamu.” Aliandika Daniel ambaye aliungwa mkono na mashabiki wake wengi.

Daniel anasoma katika chuo kikuu cha Surrey nchini Uingereza na Septemba mwaka jana baba yake (Figo), 45, aliposti picha ya binti huyo katika siku aliyojiunga na chuo hicho na akaandika “A new chaper” akionyesha kufurahishwa na hatua mpya ya binti yake huyo.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI

About Karim Boimanda

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *