Burudani

Vanesa Mdee meno nje, Albamu mambo safi sokoni

on

MWANADADA mrembo anayefanya vizuri katika muziki wa Bongo Flava hapa nchini Vanesa Mdee ‘Vee Money’ ameonyesha kufurahishwa na mapokezi mazuri ya albamu yake kwa mashabiki.

Msanii huyo alianza kuuza albamu yake kwa njia ya CD jana Mlimani City jijini Dar es salaam ambapo alisindikizwa na timu yake nzima ya Mdee Music huku mdogo wake Mimi Mars naye akiwepo.

Vanessa Mdee

Mastaa kadhaa wameonyeshwa kufurahishwa na wazo la Vanessa kutoa albamu akiwemo mpenzi wake Juma Jux, Quickracka.

Katika albamu hiyo yenye jina la ‘Money Monday’ amewashirikisha wakali kibao wakiwemo Mohombi, Joh Makini, Casper Nyovest na wengine wengi.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *