Kitaifa

+VIDEO: Azam yaifuata URA fainali

on

TIMU ya Azam FC imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya kombe la Mapinduzi baada ya kuibamiza Singida United bao 1-0 kwenye uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.

Bao pekee katika mchezo huo liliwekwa nyavuni na Shaban Idd aliyeingia kipindi cha pili na kuzima matumaini ya Singida kucheza fainali katika ushiriki wao wa mara ya kwanza kwenye michuano hiyo.

Azam wamekuwa wakionyesha kandanda safi na la mipango tangu kuanza kwa michuano hii hali inayoashiria wamepania kutetea kombe hilo walilolitwaa mwaka jana.

URA wenyewe walitangulia kutinga fainali jioni ya leo baada ya kuifunga Yanga kwa penati 5-4 hivyo sasa watapambana na Azam Januari 13.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *