Boiplus TV

+VIDEO: Bi Hindu alivyobadili gia angani na kuunga mkono mabadiliko

on

MWANACHAMA maarufu na mmoja wa wajumbe wa Baraza la Wazee la Simba, Bi Chuma Suleiman ‘Bi Hindu’ ambaye alikuwa akipinga vikali mabadiliko ndani ya Simba, leo amesema kwamba ameyapokea kwa moyo mkunjufu.

Bi Hindu alisikika mara kadhaa akipinga mabadiliko hayo ila amesema baada ya kutafakari kwa kina amegundua ni lazima mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji yafanyike kwani mpira wa miguu unahitaji pesa nyingi.

Bi Hindu

Bi Hindu akipeana mikono na Mohamed Dewji

Bi Hindu amewataka wote kumuwia radhi kwa kupinga mabadiliko hayo hapo awali na kwamba sasa wanachama wa Simba watoe ushirikiano kwa mwekezaji wao Mohamed Dewji ‘Mo’ ambaye amepita katika mchakato huo akiwa mwekezaji pekee aliyejitokeza kuomba zabuni hiyo.

“Ndio maana hata sisi tunabadilisha nguo ili tuonekane nadhifu, ni lazima Simba iende mbele na ipande juu, nimefurahishwa na haya mabadiliko, ” alisema Bi Hindu

Bi Hindu akiwaombea dua mbaya waliokuwa wakisimamia mchakato wa mabadiliko.

Bi Hindu akielezea furaha yake baada ya mchakato wa mabadili ya uendeshaji kukamilika.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI

About Sheila Ally

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *