Boiplus TV

+VIDEO: Kwasi, Mbaraka uso kwa uso Coco Beach

on

NYOTA wawili Asante Kwasi na Mbaraka Yusuf wamekutana kwenye ufukwe wa Coco wakifanya mazoezi ya utimamu wa mwili asubuhi ya leo.

Kwasi aliyesajiliwa na Simba hivi karibuni ameingia jijini Dar es Salaam jana akitokea Iringa alikokwenda kuchukua vifaa vyake kabla ya kujiunga rasmi na wenzake.

Mbaraka Yusuf na Asante Kwasi wakiwa na mdau wa Simba anayefahamika kwa jina la Tariq Hashim

Beki huyo wa zamani wa Mbao FC na Lipuli akiwa ufukweni hapo alikutana na straika wa Azam FC Mbaraka ambaye anaendelea kujiweka fit baada ya kutoka kwenye matibabu nchini Afrika Kusini.

Simba imeanza kambi jana kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ndanda lakini bado kuna mjadala kama beki huyo ajumuishwe kwenye kikosi kinachosafiri kwenda Mtwara au abaki akiendelea kujiweka sawa.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI

About Akram Msangi

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *