Kitaifa

+VIDEO: Mashabiki Arsenal wachangia damu Mwananyamala, wamuita Mo Dewji

on

MWENYEKITI wa Umoja wa mashabiki wa Timu ya Arsenal Tanzania Raymond Antony amewakaribisha kundini mashabiki wa timu hiyo akiwemo mfanyabiashara maarufu Duniani Mohamed Dewj ‘Mo’.

Akizungumza jijini Dar es salaam leo wakati wakikabidhi vifaa na kujitolea damu katika hospitali ya Mwananyamara Raymond alisema, kuna wapenzi wengi wa Arsenal hapa nchini akiwemo Mo hivyo wanamkaribisha pamoja na wengine wenye mapenzi na klabu hiyo.

Aidha Raymomd alivitaka vikundi vingine kuiga mfano wao wa kujitolea katika mambo ya kijamii ili kuwasaidia wenye matatizo mbalimbali kama wao walivyoguswa kwenda Hospitalini hapo.

Mashabiki wa Arsenal wakiwa na viti vya matairi walivyopeleka kama msaada

“Sisi kama umoja wa wapenzi wa Arsenal tumeona ni vyema kuja hapa Mwananyamala kujitolea damu na kutoa viti sita vyenye thamani ya zaidi ya sh milioni moja na hatutaishia hapa tutaendelea kujitolea zaidi na zaidi,”alisema.

Naye Muuguzi kiongozi wa zamu wa hospitali hiyo Apolina Wiliam Shirima aliwashukuru kwa kujitolea kwao huku akiwataka watanzania wengine kuiga mfano wa Umoja huo wa wapenzi wa Arsenal Tanzania.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Clezencia Tryphone

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *