Burudani

+VIDEO: Serikali yampasua kichwa Kala Jeremiah

on

MSANII anayetikisa kwa sasa na kibao chake cha ‘Kijana’ Kala Jeremiah amesema anaumiza akili yake kwa sasa ili kutoa ngoma nyingine kali ambayo itaigusa Serikali kama ilivyokuwa kwa wimbo huo.

Akizungumza na BOIPLUS, Kala alisema kitendo cha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kukubali ujumbe uliomo ndani ya wimbo huo kinazidi kumuumiza kichwa ili atoe kibao kikali na cha kuelimisha zaidi ya hicho.

‘’Nilifurahi sana kuona Makamu wa Rais anautambua wimbo wangu wa Kijana na kunipongeza kwa kazi nzuri, hivyo na mimi siwezi kumwangusha kamwe namuahidi kufanya kazi nzuri zaidi,’’alisema.

Kala aliwataka vijana wenzake kusikiliza mashairi ya wimbo huo ili waweze kupata kitu kupitia yeye kama msanii ambaye ni kioo cha jamii.

Aidha Kala alisema, mashabiki wake wakae mkao wa kula kupata vitu vizuri na vikali ambavyo vitazidi kuwajenga na kuwafunza, kwa kuwa wimbo wake wa Kijana ni maisha halisi yaliyopo kwa sasa.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *