Boiplus TV

+VIDEO: Tazama alichofanya Coutinho katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Barcelona

on

BARCELONA wamefanikiwa kumnasa Philippe Coutinho baada ya kumfukuzia kwa miezi sita lakini habari ya shughuli pevu ya nyota huyo wa kibrazili wanayo tangu miaka sita iliyopita.

Coutinho aliyekuwa akiitumikia Inter Milan alitumia muda mwingi wa msimu wa 2011/12 akiwa kwa mkopo katika klabu ya Espanyol inayoshiriki ligi kuu nchini Hispania ‘La Liga’.

Espanyol ndio wapinzani wakuu wa Barcelona katika jimbo la Katalunya na akiwa kikosini hapo alipata nafasi ya kucheza ‘Derby’ yake ya kwanza akiingia dakika 66 na kufanikiwa kucheza dakika 25 ambazo mashabiki wa Barcelona hawaachi kuzikumbuka kutokana na uwezo mkubwa aliouonyesha siku hiyo.

Katika mechi hiyo ambayo ilikuwa ya mwisho ya nyumbani kwa kocha Pep Guardiola kabla hajaondoka klabuni hapo, Barcelona waliibuka na ushindi wa mabao 4-0 yote yakiwekwa nyavuni na Lionel Messi.

Baada ya miaka sita kupita tangu tukio hilo, Coutinho yupo tena Barcelona safari hii akiwa mchezaji katika klabu ya ndoto zake kama alivyoeleza siku aliyotambulishwa.

Tazama video hii hapa uone alichofanya Coutinho siku hiyo.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *