Boiplus TV

+VIDEO: Wachezaji Sweden wavunja meza wakishangilia kwenda Urusi

on

NI ngumu sana kuizuia furaha ingawa kuna wakati usipoizuia inaweza kusababisha matatizo, hili ndilo lililotokea jana pale wachezaji wa timu ya taifa ya Sweden walipovunja meza ya kituo cha televisheni cha Eurosport.

Tukio lilitokea kwenye uwanja wa San Siro wakati nyota hao wakiwa katika ‘sherehe’ za kufuzu kwa fainali za kombe la dunia zitakazofanyika mwakani nchini Urusi.

Mtangazaji wa Eurosport alikuwa akiendelea na mahojiano katika meza iliyowekwa pembeni ya uwanja jirani na kibendera cha kona ndipo kundi la wachezaji hao lilipomvamia na kusababisha meza hiyo kuvunjika.

Sweden walifuzu baada ya kuilazimisha Italia sare ya bila mabao hivyo kuwafanya wawalize waitaliano kwa jumla ya bao 1-0 walilolipata kwenye uwanja wao wa nyumbani katika mchezo wa kwanza.

 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *