Trending (Kijamii)

VITUKO MSIBA WA IVAN: Mahakama Yaamuru Pesa Zote Zilizofukiwa Zitolewe Watu ‘Wakazitumbue’

on

KAMPALA, Uganda
MAHAKAMA kuu nchini Uganda imewataka ndugu wa marehemu Ivan Semwanga ‘Ivan The Don’ kuufukua mwili wa mfanyabiashara huyo na kutoa pesa alizozikwa nazo ili kulinda heshima ya pesa ya nchi hiyo na nchi washirika.

Ivan 39, ambaye alizaa watoto watatu na Zari anayeishi na msanii nyota wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platinum kwa sasa, alizikwa Mei 30 jijini Kampala baada kufariki nchini Afrika Kusini alipokuwa amelazwa kwenye hospitali ya Steve Biko jijini Pretoria.

Kabla ya mwili wa mfanyabiashara huyo kijana haujaingizwa kwenye kaburi matajiri wenzake walianza kumwaga pesa nyingi na baadae wakaingiza mwili na kufunikia kitu ambacho Mahakama hiyo imeona kama ni kuishusha thamani pesa ya nchi hiyo na nchi washirika.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mahakama hiyo leo Juni 2 pesa zilizozikwa pamoja na mwili wa marehemu ni shilingi ya Uganda, Randi ya Afrika Kusini pamoja na Dola za Marekani.

Mahakama hiyo imewataka ndugu wa marehemu kufukua kaburi kwa gharama zao na kuzitoa pesa zote ili ziendelee na mzunguko kwakua pesa ni mali ya Serikali.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *