Kitaifa

Wachezaji Simba warejea na kupewa mapumziko wakaiwaze ligi kuu

on

BAADA ya kikosi cha Wekundu wa Msimbazi Simba, kurejea leo mchana kikikotea visiwani Zanzibar, nyota wake wamepewa mapumziko ya siku mbili ili warejee wakiwa fit kwa ajili ya mechi za ligi kuu.

Simba imerejea mchana wa leo, baada ya kufungashiwa virago katika michuano ya kombe la Mapinduzi inayoendelea kutimua vumbi visiwani humo, wakikubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa URA.

Akizungumza na BOIPLUS kocha wa Wekundu hao, Masoud Djuma alisema nyota wake watapata mapumziko ya siku mbili na Alhamis watarejea na kuendelea na mazoezi kama kawaida.

Djuma alisema, matokeo waliyoyapata katika mchezo wa jana yaliwaumiza kwani matarajio yao ilikuwa ni kurejea na kombe la michuano hiyo.

Wakati huo huo, nahodha wa kikosi hicho John Bocco amewataka wanasimba kuendelea kuwasapoti kwani hata wao hawajafurahishwa na matokeo hayo.

“Binafsi hata sisi wachezaji hatujapendezwa kabisa na matokeo haya, ila ndio mpira una matokeo ya aina tatu ambayo ni sare, kushinda au kufungwa,” alisema Bocco na kuongeza kuwa wanaganga yajayo kwa sasa kwani wana mechi nyingi mbeleni ikiwemo inayofuata dhidi ya Singida United.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Clezencia Tryphone

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *