Kitaifa

Wachezaji wawili tu wamesalia Stand vs Yanga leo

on

NI takribani siku 392 tangu timu za Stand United na Yanga zipambane kwenye uwanja CCM Kambarage katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2016/17.

Hii ni sawa na mwaka mmoja na siku kama 27 tangu tushuhudie Pastory Athanas akiwanyamazisha maelfu ya mashabiki wa Yanga kwa bao pekee lililoipa ushindi Stand iliyokuwa chini ya kocha mzungu Patrick Liewig.

Wakati Yanga wanakwenda Shinyanga kuwavaa wapiga debe hao, walikuwa hawajapoteza mchezo wowote wakishika nafasi ya pili kwa pointi zao 10 kwenye msimamo wa ligi uliokuwa ukiongozwa na wekundu wa Msimbazi, Simba ambao walikuwa na pointi 16.

Ushindi huo dhidi ya Yanga uliwafanya Stand wafikishe pointi 12 zilizowapandisha hadi nafasi ya pili huku Yanga wakishuka hadi nafasi ya tatu. Lakini kuelekea mchezo wa leo hali ni tofauti kabisa, Stand wapo nafasi ya 14 wakiwa na pointi nne tu huku Yanga wakiwa nafasi ya nne baada ya kujikusanyia pointi 12.

Baada ya kupoteza mchezo huo, Yanga walisafiri hadi kisiwani Pemba kujiwinda na mchezo dhidi ya watani zao wa jadi Simba ambapo mchezo wao ulimaliza kwa sare ya bao moja, Amissi Tambwe na Shiza Kichuya wakizifungia timu zao. Taarifa zinasema baada ya mchezo wa leo Yanga watarejea tena Pemba kwa ajili ya mechi ya watani Oktoba 28.

Umebakia muda mfupi Yanga wapepetane na Stand katika mchezo wa kisasi na tayari makocha wa timu zote mbili wameshatangaza vikosi vitakavyoanza leo.

Jambo la ajabu na la kipekee ni kwamba ni wachezaji wawili pekee ambao walianza katika pambano la Septemba 25 mwaka jana ndio wataanza tena kwenye vikosi vya kwanza vitakavyoanza mchezo wa leo.

Wachezaji hao ni beki Erick Mulilo wa Stand United na Andrew Vicent ‘Dante’ wa Yanga huku baadhi wakianzia benchi leo. Haya ni mabadiliko makubwa ambayo yanaweza kubadili kila kitu katika mchezo huo wa kukata na shoka.

Kikosi cha kwanza cha Stand United katika mchezo huo kilikuwa hivi;
1. Frank Mwamongo
2. Revocatus Richard
3. Adeyum Ahmed
4. Erick Mulilo
5. Ibrahim Job
6. Jacob Masawe
7. Pastor Athanas
8. Geremy Katura
9. Kelvin Sabato
10. Suleiman Kassim ‘Selembe’
11. Adam Kingwande

 

Kikosi cha kwanza cha Yanga SC kilikuwa;
1. Ally Mustafa ‘Barthez’
2. Juma Abdul
3. Mwinyi Hajji
4. Vincent Bossou
5. Andrew Vincent
6. Mbuyu Twite
7. Simon Msuva
8. Thabani Kamusoko
9. Donald Ngoma
10. Amissi Tambwe
11. Deus Kaseke

Kikosi cha kwanza cha Stand United leo ni;
GK-Frank Muwonge-30
2. Aron Mokoena-23
3. Hamad Kibopile-28
4. Erick Mulilo-13
5. Ally Ally-9
6. Rajab Rashid-3
7. Ambros James-29
8. John Mwitiko-20
9. Adam Salamba-10
10. Wisdom Mutasa-21
11. Emmanuel Kitoba-26

 

Kikosi cha kwanza cha Yanga SC leo ni;
GK-Youthe Rostand-30
2. Hassan Hamis-25
3. Gadiel Michael-2
4. Andrew Vicent-28
5. Nadir Haroub-23
6. Pato Ngonyani-15
7. Pius Buswita-3
8. Papy Tshishimbi-25
9. Obrey Chirwa-7
10. Ibrahim Ajib-10
11. Geoffrey Mwashiuya-19

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *