Kitaifa

Yanga kuzilipia ‘madeni’ Simba, Azam?

on

USIKU wa Jumatatu Yanga iliambulia sare ya bao moja dhidi ya Singida United katika mchezo wa kutafuta heshima ya kuongoza kundi B kati ya timu hizo kutoka Tanzania Bara.

Hadi zinaingia katika mchezo huo Singida na Yanga zilikuwa zimeshafuzu sawa na Azam kutoka kundi A ambalo lilikuwa likisubiri matokeo ya mchezo kati ya Simba na URA ili kujua nani wa kuungana na Azam ambapo URA walifanikiwa kufuzu.

Wakusanya kodi hao wa Uganda wamemaliza wakiwa vinara wa kundi A hivyo kulazimika kukutana na Yanga walioshika nafasi ya pili katika kundi B huku Azam wenyewe wakiumana na Singida United.

Yanga inaenda kukutana na URA ambayo imefanikiwa kuvituliza vigogo Simba na Azam kwa kichapo cha bao moja kila mmoja, swali ni je Yanga watafanikiwa kuwalipia kisasi vigogo hao au na wao wataingia mkumbo wa kuadhibiwa?

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *