Afrika

Zanzibar noma, waivua ubingwa Uganda na kutinga fainali CECAFA

on

TIMU ya Taifa ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’ imeivua ubingwa wa michuano ya Cecafa Uganda Cranes baada ya kupata ushindi wa bao 2-1.

Zanzibar Heroes ni miongoni mwa timu ambazo hazikutarajiwa kufika hatua hiyo lakini baada ya ushindi wa mechi zake za hatua ya makundi ilianza kuhofiwa kutokana na uwezo wao kisoka.

Waandaaji wa mashindano hayo nao waliingiwa na hofu juu ya kiwango cha wachezaji wa Zanzibar hadi kufikia uamuzi wa kuchukuwa vipimo ili kujua kama wanatumia dawa za kuongeza nguvu, majibu ambayo hadi sasa bado hayajatangazwa.

Zanzibar sasa watacheza fainali keshokutwa Jumapili dhidi ya wenyeji Harambee Stars ambao waliifunga Burundi bao 1-0 hatua ya nusu fainali mechi iliyokwenda hadi dakika ya 120 baada ya kutoka sare tasa katika dakika 90.

Nyota Abdulazizi Makame (pichani) ndiye alikuwa wa kwanza kutikisa nyavu za wapinzani wao dakika ya 22 huku Uganda ikijibu mapigo dakika ya 27 kupitia kwa Nsibambi Derrick kabla Mohamed Issa hajaipatia Zanzibar bao la ushindi dakika ya 57 kwa mkwaju wa penalti.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI

About Sheila Ally

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *