Kitaifa

ZIMBWE JR: Zingekuwa Mbili, Moja Ningempa Mzamiru

on

MCHEZAJI bora wa Simba msimu wa 2016/17 Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amewashukuru mashabiki, viongozi na wachezaji wenzake kwa tuzo hiyo lakini akasema kama zingekuwa zipo mbili basi moja angempa Mzamiru Yassin.

Akizungumza na BOIPLUS MEDIA leo Zimbwe alisema waliotoa tuzo wanafahamu kwanini wamempatia yeye lakini anaamini kama kungekuwa na nafasi ya kwanza na ya pili basi nyota mwingine aliyepaswa kupewa tuzo hiyo ni Mzamiru.

“Nashukuru nimeshinda tuzo hii, itaniongezea morali, lakini kiukweli Mzamiru pia angestahili kupata baada ya mimi, sema kwavile inakuwa moja basi ndio sababu yeye hajapata.

“Amecheza mechi nyingi na kuisaidia sana timu kupata matokeo yaliyotufikisha hapa tulipo, kwa upande wangu huyu pia ni mchezaji bora kabisa,” alisema beki huyo wa kushoto aliyecheza michezo yote ya ligi kuu msimu huu.

Zimbwe ambaye usiku wa leo anawania tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom pamoja na nyota Simon Msuva na Haruna Niyonzima (Yanga), Shiza Kichuya (Simba) pamoja na Aishi Manula (Azam) ametwaa tuzo hiyo kwa ngazi ya klabu ambayo imetangazwa asubuhi ya leo.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *