The sports Hub

MAKAMBO: Idadi ni Siri Yangu Ila Wataziokota Sana ‘Kunyavu’

0 175

MKONGOMANI wa Yanga Heritier Makambo, amesema hawezi kuweka wazi ni idadi ipi ya mabao aliyojipangia kukifungia kikosi chake katika msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ila anakiri kwamba malengo yake ni kufunga mabao mengi kwa kutumia vema kila nafasi anayoipata.

Straika huyo aliyeletwa na kocha Mwinyi Zahera alisema wachezaji wengi hupenda kutaja mapema kila kitu walichojipangia lakini yeye ni tofauti kwani anataka watu waone waseme na si yeye kuwaambia.

Heritier Makambo

“Siwezi kuweka wazi ni idadi ipi ya mabao nahitaji lakini nahitaji kufunga mabao mengi sana halafu kama ni kiatu cha mfungaji bora kitanifuata chenyewe,” alisema Makambo.

Makambo mwenye mabao 11 aliongeza kuwa yeye ni mchezaji ambaye hana mpinzani katika uchezaji wake, anamwamini Mungu katika kila hatua ambayo anaipitia na jukumu lake kubwa muhimu kwake ni kuhakikisha timu yake inapata ubingwa msimu huu.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.